Friday, December 19, 2025
spot_img
HomeMichezoUCHAMBUZI: Simba Sc mara sita mfululizo wamepoteza mechi dhidi ya Yanga Sc

UCHAMBUZI: Simba Sc mara sita mfululizo wamepoteza mechi dhidi ya Yanga Sc

Kwenye hizo mechi sita walizopoteza kuna baadhi ya mechi waamuzi wamekua sehemu ya Yanga Sc kupata matokeo chanya.

Nina reference ya mechi tatu za msingi ambazo kwa namna moja ama nyingine waamuzi moja kwa moja hawakwepi lawama.

Tuanze na ya jana, Arajiga na line 1 wameipa Yanga Sc goli ambalo Kwangu naona halikupaswa kuwa goli.

Kelele zimekua kuhusu Pacome Zouazoua kuwa kwenye Offside position, ukirejea kwenye kanuni 17 za mpira wa miguu,sheria namba 11 inaongelea offside (kuotea).

Kuwa kwenye Offside position sio shida,shida ni mchezaji kuingilia mchezo, Pacome hakuingilia mchezo lakini tukio la pili ambalo kwangu naona kama Mohamed Mkono alipaswa kun’gamua, wakati Max Nzegeli anafanya movement Shomari Kapombe alikua ndio ana m mark, wakati huo Rushine De Reuck nae akifanya runs lengo likiwa kusahihisha endapo Kapombe angeshindwa kumzuia Max ,ndio Pacome Zouazoua akafanya Obstruction kwa Rushine ( hii ilapaswa kuwa faulo kuelekea Yanga Sc) kwasababu Pacome alifanya madhambi.

Kuna mechi refa akiwa Arajiga, Yanga Sc walishinda goli 1-0 ,goli la Max Nzegeli.

Lakini wakati mpira ukiwa unaelekea mwishoni (dakika ya 89 hivi) Chadrack Boka alimvaa Kelvin Kijili ndani ya box lakini refa akameza filimbi.. ilikua clear penalty kabisa.

Mechi nyingine refa akiwa Ramadhan Kayoko kuna matukio mawili ambayo Kibu Dennis alikwatuliwa ndani ya box.

Alikwatuliwa na Chadrack Boka
Alikwatuliwa na Mudathir Yayha

Kwenye mazingira yale, Simba Sc ilipaswa kunufaika na pigo la penalty.

Unakumbuka kile kipigo cha magoli 5-1?

Inawezakana magoli yalikua mengi kufungwa Simba Sc lakini Ahmed Arajiga huyu huyu aliona tukio akiwa karibu lakini alimeza filimbi na Yanga Sc kufunga goli.

Ilikua tukio la rafu mbaya ya Mudathir Yayha kumchezea Sadio Kanoute ila Arajiga

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments