Saturday, March 14, 2026
spot_img
HomeHabariUN yaonyesha tena matumaini makubwa Tume ya Jaji Chande

UN yaonyesha tena matumaini makubwa Tume ya Jaji Chande

* Tume ya Jaji Mohmed Chande yang’ara duniani

‎*UN yakoshwa tena na  Tume ya uchunguzi ya Jaji Mohmed Chande

‎*Heshima ya Tume ya Jaji Chande yazidi kuikosha UN


‎Geneva, Uswisi

‎Msimamizi maalumu wa Umoja wa Mataifa (UN), Gina Romero, ameisifu Tanzania kwa kuunda Tume huru ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba, kuwa ni uthibitisho kujali haki za binadamu.

‎Gina aliisifu Tanzania mjini Geneva, Uswisi,  Machi 12, alipofanya majumuisho ya mada  kuhusu : Ukweli na Uwajibikaji katika Matukio ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 nchini Tanzania.

‎Katika majumuisho hayo, Gina  alisema Tume hiyo ya Jaji Mkuu mstaafu Mohmed Chande, ni ishara nzuri ya Tanzania kujali haki za binadamu na kuamua kufanya uchunguzi huru.

‎Tayari pia Tume hiyo ilisifiwa na Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), Volker Turk, alipofungua kikao cha 61 cha baraza hilo, mjini Geneva, Uswisi, wiki iliyopita.

‎Tume hiyo imekuwa ikiungwa mkono kutokana na weledi na uadilifu wa Jaji Mkuu mstaafu Chande, ambaye UN imekuwa ikimtumia katika uchunguzi ukiwemo wa tuhuma za mauaji holela katika Mji wa  el Fasher, Sudan.

‎Pia, Jaji Chande aliwahi kuongoza jopo la  uchunguzi wa tukio la ajali ya ndege lililomuua Katibu Mkuu wa UN, Dag Hammarskjöld.

‎AMNESTY, HRW KIKAANGONI

‎Taarifa ya ukosoaji huo uliyotolewa wa Machi 12, imekuja kipindi ambacho Amnesty International (AI) na Human Rights Watch (HRW), zikikiri kuandaa ripoti za upande mmoja zaidi katika matukio ya Oktoba 29, mwaka jana.

‎Majibu ya serikali ya Tanzania yalitokana na hoja potofu za AI na HRW, kudai kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu katika kudhibiti vurugu za uchaguzi.

‎Hata hivyo, madai hayo potofu yalitolewa ufafanuzi na serikali katika kikao hicho cha 61 cha UNHRC, na kuungwa mkono na wadau wengine wakiwemo kutoka Zimbabwe, ambao walihoji weledi na uadilifu wa AI na HRW katika kuandaa ripoti zao.

‎Katika kupinga madai hayo, AI na HRW ziilikosolewa kuwa ripoti zao wanaziandaa kwa msukumo wa kisiasa badala ya kutoa haki kwa pande mbili kwa lengo la kupata ukweli.

‎Taarifa ya serikali ya Tanzania ilizikosoa taasisi hizo mbili kwa upendeleo wa kisiasa, kufumbia macho walioanzisha, kuchochea vurugu, kutopata taarifa sahihi na kutothamini mchango wa vyombo vya usalama katika kulinda usalama wa nchi, watu na kusimamia utawala wa sheria dhidi ya waliotaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

‎Pia, taarifa hiyo ya serikali ilifafanua kuwa katika kipindi cha uchaguzi mitandao ya kijamii ilijaa taarifa nyingi za kupandikiza chuki, vurugu na hata kauli za kihaini kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, watu binafsi na taasisi za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi.

‎Tanzania ilihoji ni vipi matukio hayo yote hayamo katika ripoti za Amnesty International na Human Rights Watch.

‎Katika wasilisho hilo, Tanzania iliomba Amnesty International na Human Rights Watch zitoe mwongozo wa wazi na mapendekezo; ni nguvu kiasi gani zilipaswa kutumika kulinda maisha ya watu na kulinda utawala wa sheria na mamlaka ya dola dhidi ya watu waliokataa kutii amri halali.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments