Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka amesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Said Mwema kuwa Mjumbe wa Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani Oktoba 29, umetokana na uzoefu wake.
Ameutaja uzoefu huo, akisema Mwema amewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania na katika kipindi chake, alisimamia marekebisho makubwa ya jeshi na kuandaa mkakato wa polisi jamii.
Amesema akiwa na wadhifa huo, aliliongoza jeshi hilo kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo wa kuvuka mipaka, dawa za kulevya na ujambazi.
Sambamba na nafasi hiyo, amesema Mwema amewahi kuwa Mkuu wa Kanda Ndogo ya Interpol ya Nairobi na alikuwa Mjumbe katika Tume ya Kurekebisha Mifumo ya Haki Jinai.




