Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeBiasharaVodacom yaendelea na kampeni ya Sikukuu, kurudisha kwa jamii

Vodacom yaendelea na kampeni ya Sikukuu, kurudisha kwa jamii

Vodacom Tanzania PLC leo imezindua rasmi msimu wa sikukuu, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea na kushirikiana na jamii, huku kampuni hiyo ikihitimisha maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Kupitia kampeni hii, Vodacom inasisitiza kaulimbiu yake ya “Tupo Nawe Tena na Tena” kwa kuwazawadia wateja, kueneza furaha na kuimarisha mahusiano katika msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, alisema msimu huu sio tu wa kusherehekea, bali pia kuendeleza dhamira ya kampuni katika kuboresha uzoefu wa mteja na kuleta maendeleo jumuishi.

“Vodacom imebadilisha maisha kupitia mtandao wake mpana na ubunifu. Msimu huu wa sikukuu tunasherehekea wateja, washirika na jamii zinazofanikisha safari yetu. Tunabaki kuwa mtandao bora unaowaunganisha watu na wapendwa wao,” alisema Besiimire.

Kwa upande wake, Brigita Stephen, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko (CBU), alisema kampeni hiyo inalenga kuwafikia wateja moja kwa moja kupitia usambazaji wa makapu 600 ya sikukuu yenye mahitaji muhimu pamoja na ofa mbalimbali kwa watumiaji wa M-Pesa.

“Kampeni yetu inalenga kumweka mteja mbele, ikitoa unafuu, urahisi na thamani. Kupitia mpango wa Makapu, tunarudisha kwa jamii huku tukiwashukuru wateja wetu ambao wamekua nasi kila hatua,” alisisitiza Brigita.

Akifafanua zaidi kuhusu ofa za msimu, Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa, alieleza kuwa watumiaji watapata punguzo la 50–100% kwenye tiketi za SGR katika siku maalum, mafuta ya bure lita mbili kwenye vituo vilivyobainishwa, pamoja na cashback ya hadi 10% kwenye malipo katika maduka makubwa na huduma za chakula na malazi (HoReCa).

“M-Pesa inaendelea kufanya malipo ya sikukuu kuwa rahisi, nafuu na yenye faida. Ofa hizi zinaongeza thamani na kuimarisha mfumo wa malipo ya kidijitali nchini,” alisema Mbeteni.

Kwa upande wa wafanyabiashara wadogo na wa kati, Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Vodacom Business, alitangaza punguzo maalum ikiwemo upunguzaji wa 15% kwenye bei za vifurushi vya ujumbe mfupi (SMS) kwa wingi, miezi miwili ya usajili bure kwa huduma ya ufuatiliaji magari, na punguzo la 20% kwenye vifaa vya ufuatiliaji.

“Vodacom Business inaendelea kuwa mshirika mkuu wa biashara na watu binafsi, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu,” alisema Kamando.

Kwa ujumla, kampeni ya msimu wa sikukuu ya Vodacom Tanzania inaonesha dhamira ya kampuni kuendelea kuwaunganisha watu, kuimarisha maisha ya kidijitali na kuendeleza maendeleo kwa kutoa huduma na ofa zinazogusa wateja wote—kuanzia kaya, biashara hadi jamii kwa ujumla.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments