Saturday, March 14, 2026
spot_img
HomeBiasharaWachimbaji wadogo Mbogwe washauriwa kufuata kanuni za msaada wa kiufundi‎

Wachimbaji wadogo Mbogwe washauriwa kufuata kanuni za msaada wa kiufundi‎

Wachimbaji wadogo wa madini  Mkoa wa kimadini Mbogwe wametakiwa kuzingatia Kanuni za Msaada wa Kiufundi  zilizotangazwa na Serikali ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuepuka migogoro isiyo ya lazima na wawekezaji.

‎Rai hiyo ilitolewa Machi 13, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa  wakati wa ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Peter Kisura Kawe na Washirika uliopo wilayani Mbogwe.

‎Dk. Kiruswa alisema kuwa ni vyema kuzingatia Kanuni mpya za mwaka 2025 zinazoratibu ushiriki wa watoa msaada wa kiufundi katika leseni ndogo za uchimbaji.

‎Dk.Kiruswa alieleza kuwa , mikataba yote ya msaada wa kiufundi kati ya mchimbaji mdogo na mtoa huduma lazima isajiliwe rasmi Tume ya Madini.

‎Dk.Kiruswa alifafanua kuwa kanuni zinaelekeza kuwepo kwa uwazi katika mgawanyo wa mapato ya madini yatakayozalishwa ili kumlinda mchimbaji mdogo.

‎Aliongeza kuwa , msaada wa kiufundi  unapaswa kulenga kuongeza ujuzi, kutoa teknolojia ya kisasa, na kuongeza kiasi cha madini kinachopatikana.

‎Dkt.Kiruswa alisisitiza kuwa,wachimbaji wadogo wana fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia programu maalum za kibenki kama CRDB Bank zilizozinduliwa hivi karibuni.

‎Kwa upande wake Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa kimadini Mbogwe Mhandisi Ludovick Mwacha alisema mpaka sasa mkoa wa kimadini Mbogwe umefikia asilimia 75.81 makusanyo ya lengo la Mwaka 2025/2026.

‎Awali, akitoa taarifa ya mwenendo wa uzalishaji katika mgodi wa Peter kisura na Washirika , Meneja Mgodi  Mhandisi  Samson Mathias  alisema, mgodi ulianza  uzalishaji rasmi  mwaka 2025 na mpaka sasa unazalisha kilogram 8 kwa mwezi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments