Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeElimuWanafunzi 6,000 kuanza kidato cha kwanza 2026 bila kikwazo

Wanafunzi 6,000 kuanza kidato cha kwanza 2026 bila kikwazo

Manispaa ya Kibaha imetenga Sh milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kujiunga na masomo mwaka 2026.

Aidha, imetenga Sh milioni 400 kwa ajili ya kutengeneza madawati kwa shule za sekondari za manispaa hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dk. Mawazo Nicas, ametoa taarifa hizo Desemba 10 wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisema maandalizi hayo ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi watakaojiunga na elimu ya sekondari.

Kwa mujibu wa Dk. Nicas, wanafunzi 6,000 walifaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, sawa na asilimia 100—ongezeko kubwa ikilinganishwa na wanafunzi 3,050 waliofaulu mwaka uliopita.

Wanafunzi wote waliomaliza darasa la saba watajiunga na kidato cha kwanza. Hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi mwaka 2026,” amesema.

Ameongeza kuwa ndani ya siku 60 ujenzi wa madarasa utakamilika ili wanafunzi waanze masomo kwa wakati. Kuhusu madawati, amesema mzabuni tayari amepewa kazi ya kuyatengeneza ili yakamilike kabla ya muda wa kuanza kwa mwaka wa masomo.

Aidha, Meya huyo amesema Manispaa itaendelea kuhakikisha kuwa watoto wote wa darasa la kwanza wenye umri wa kuandikishwa wanaanza shule kama taratibu zinavyoelekeza.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments