Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariWasifu wa Jaji Mohamed Chande Othman

Wasifu wa Jaji Mohamed Chande Othman

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka ameutaja wasifu wa Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani, Jaji mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa mzoefu katika tasnia ya sheria.

Sio tasnia ya sheria pekee, amesema ni mzoefu pia hata katika utoaji haki hasa za binadamu kitaifa na kimataifa, huku akiwa na uelewa mpana wa masuala ya utunzaji wa amani duniani.

Jaji Chande pia, amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania hadi mwaka 2017, kadhalika Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa Balozi Kusiluka, Chande pia amewahi kuwa kiongozi wa tume ya uchunguzi wa machafuko ya Sudan na Mjumbe wa tume huru ya kutathmini utendaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Pia, amewahi kuwa mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu nchini Rwanda na amewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Mifumo ya Haki Jinai.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments