
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema watu watatu wamefariki dunia baada ya kuungua moto katika eneo la ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Korogwe Fuel katika Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga , Almachius Mchunguzi amesema walipokea taarifa ya ajali hiyo Septemba 23, 2024 majira ya saa 03:45 usiku, na baada ya uchunguzi wa awali wa miili iliyokuwa nje ya gari ilibainika ni ya jinsia ya kike na ndani ya gari kiti cha nyuma ulionekana mwili mwingine ambao haukutambulika kutokana na kuungua.