Timu 20 kutoka Unguja na Pemba zimefuzu hatua ya pili ya ZFF FA Cup baada ya kufanya vizuri katika hatua ya awali ya mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).
Katibu wa Kamati ya Mashindano, Ali Bakari, amesema timu hizo sasa zitakutana na klabu 12 za Ligi Kuu Zanzibar kwenye hatua ya 32 Bora.
Amesema mfumo wa kanda umetumika kutokana na changamoto za gharama za usafiri kwa baadhi ya timu, huku juhudi za kutafuta wadhamini zikiendelea.
Timu zilizofuzu ni:
Kwerekwe FC, Pete Star, Taifa Jang’ombe, New Power, Inter Zanzibar, Paje Star, Mwakaje Star, Jobless, Muembe Makumbi Utd, Raskazone, Muungano Ranger, Maungani, Urafiki, New City, Ujamaa, Negro United, Bweleo Warriors, Kinuni Star, Black Sailors na Kundemba.




