Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariMabalozi wathibitisha kuimarisha ushirikiano na Tanzania

Mabalozi wathibitisha kuimarisha ushirikiano na Tanzania

Mabalozi wanaowakilisha mataifa na taasisi za kimataifa nchini wamethibitisha kwa kauli moja dhamira yao ya kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali, hususan ya kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa leo, Ijumaa Novemba 28, 2025, wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaohudumu nchini.

Wanadiplomasia hao wamesema wanaiona Tanzania kama mshirika muhimu, imara na mwaminifu katika diplomasia ya kikanda na kimataifa. Aidha, wametambua juhudi zinazofanywa na Serikali katika kurejesha umoja wa Taifa kufuatia matukio ya Oktoba 29, na wamepongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha amani, utawala bora na ustahimilivu wa kitaifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi Kombo aliwahakikishia mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano wa manufaa kwa pande zote.

Alitumia fursa hiyo kuwapa taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu, matukio yaliyotokea baadaye, na hatua zilizochukuliwa na Serikali — ikiwemo kulinda maisha na mali za wananchi, kurejesha utulivu, pamoja na kuendeleza huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi bila kusita.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments