
Viongozi Wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo wanatarajia kufanya awamu ya pili ya ziara ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inayotarajiwa kuanza Septemba,11 2024.
Awamu ya kwanza ya ziara hiyo ya #Miezi10 #WanachamaMilioni10 ilifanyika kuanzia Julai 22, 2024 hadi Agosti 17,2024 ikihusisha majimbo 125 yaliyopo katika mikoa 22.
Kama ilivyokuwa kwenye awamu ya kwanza ya ziara, awamu ya pili itawahusisha Kiongozi wa Chama Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti Isihaka Mchinjita, Katibu Mkuu Ado Shaibu na Kiongozi wa Chama Mstaafù Zitto Kabwe kama ifuatavyo;

1.Kiongozi wa Chama Dorothy Semu atatembelea maǰimbo 25 kwenye Mikoa ya Pwani, Dodoma, Manyara, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

- Makamu Mwenyekiti Bara Isihaka Rashid Mchinjita atatembelea majimbo 21 katika MiÄ·oa ya Dar es Salaam na Morogoro.

3. Katibu Mkuu Ado Shaibu atatembelea Majimbo 29 katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Geita, Mwanza, Simiyu, Kagera na Mara.

5. Kiongozi wa Chama Mstaafu Zitto Kabwe atakuwa na ziara kwenye Majimbo 29 ya Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya na Songwe.
Malengo ya Awamu ya Pili ya Ziara ni kama ifuatavyo;
- Kuendelea kuimarisha Chama kilichoenea Tanzania Bara na Zanzibar katika kona zote za Tanzania. Huu ni utekelezaji wa Agizo la Halmashauri Kuu ya Chama kuwa kabla ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni lazima viongozi wakuu wa Chama wafanye ziara kwenye kila Jimbo katika Majimbo yote 214 ya Tanzania
Bara. Ziara hii ya awamu ya pili inakamilisha utekelezaji wa agizo hilo. - Kukagua utekelezaji wa Azimio la Halmashauri Kuu ya Chama la kuhakikisha kila Kitongoji, Kijiji na Mtaa kina mgombea wa ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Halmashauri Kuu ya Chama imeagiza Chama kisimamishe wagombea kwenye vitongoji, vijiji na mitaa yote nchini. Ziara hii inakwenda kuhakikisha hakuna kitongoji, kijiji wala mtaa wowote unakwenda kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za
Mitaa bila kuwa na mgombea wa ACT Wazalendo.
Wanachama 418,000 wameandaliwa kuwa wagombea katika ngazi mbalimbali zinazogombewa katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
- Kuhamasisha kampeni ya Chama ya kusajili wanachama Milioni 10 kwa miezi 10 ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 22 Julai 2024. ACT Wazalendo imejiwekea lengo la kuwa Chama chenye idadi kubwa zaidi ya wanachama nchini ifikapo mwezi
Aprili, 2024. - Kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitolea majawabu kwa kuzingatia ahadi
ya ACT Wazalendo kwa Watanzania ya Taifa la Wote, Maslahi kwa Wote