Airtel Tanzania imeungana na mataifa mengine kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka 2025, chini ya kaulimbiu ya “Mission Possible” (Dhamira Inawezekana), inayolenga kuimarisha falsafa ya kampuni ya “Mteja Kwanza.” Kaulimbiu hii inaendana na dhamira ya Airtel katika kuhakikisha huduma bora, za ubunifu na zinazoweka mteja katika kiini cha shughuli zake zote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, amesema maadhimisho ya wiki hii yanatambua, kushukuru na kuthibitisha dhamira ya kampuni katika kuboresha huduma kwa wateja. “Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka huu si maadhimisho ya muda mfupi tu, bali ni fursa ya kuimarisha utamaduni wetu wa kuweka mteja kipaumbele chetu cha kwanza kupitia vituo vyetu, idara za huduma kwa wateja na timu ya uongozi,” amesema Kamoto.

Kwa mwaka uliopita, Airtel Tanzania imeendelea kuwekeza katika ubunifu na huduma zinazorahisisha maisha ya wateja, ikiwemo LUKU Token Retrieval, ambayo imewezesha maelfu ya wateja kupata namba zao za LUKU kwa urahisi na kuepuka kukatika kwa umeme. Huduma za kujihudumia (self-care tools) pia zimewapa wateja uwezo wa kusimamia akaunti zao kwa uhuru na urahisi zaidi.
Airtel pia imekuwa ikishirikiana kwa karibu na wateja ili kuelewa mahitaji yao yanayobadilika. Kupitia mrejesho wa moja kwa moja, kampuni imeboresha huduma zake na kuimarisha uhusiano na jamii. Upanuzi wa mtandao wa vituo vya huduma umelenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi, mijini na vijijini, kwa huduma zenye ubora na ukaribu.
Miongoni mwa shughuli za maadhimisho, Airtel imeandaa namna mbalimbali za kuwashukuru wateja kupitia maduka na majukwaa ya kidijitali, ikithibitisha imani na uaminifu wao. Huduma mpya za kujihudumia, kama self-reversal, zinaruhusu wateja kurekebisha muamala uliofanyika kimakosa bila kwenda kwa wakala au ofisini, na kupata udhibiti kamili wa akaunti zao za Airtel Money.
Airtel Tanzania inaendelea kushirikisha wateja wake na kuthibitisha kuwa kaulimbiu ya “Mteja Kwanza” si maneno tu, bali ni ahadi ya kuboresha huduma kila siku, kukuza ubunifu, na kufanya maisha ya kila Mtanzania anayechagua Airtel kuwa bora na rahisi zaidi.





