Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeBiasharaBenki ya Exim, Simba Developers waingia makubaliano umiliki wa nyumba

Benki ya Exim, Simba Developers waingia makubaliano umiliki wa nyumba

Dar es Salaam, 28 Novemba 2025: Benki ya Exim Tanzania na Simba Developers Limited wametia sahihi ya makubalianio ya kimkakati yanayolenga kurahisisha upatikanaji wa makazi kwa Watanzania.

Ushirikiano huu unalenga kutoa suluhisho la mikopo ya makazi yenye masharti rahisi kwa wateja wanaponunua nyumba za kisasa zilizojengwa na Simba Developers, kupitia bidhaa ya mkopo ya Exim Bank iitwayo ‘Nyumba Yangu’.

Ushirikiano huu umelenga kujibu ongezeko la mahitaji ya mikopo ya makazi ya bei nafuu katika maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji, ambapo wamiliki wengi wa nyumba wanakabiliwa na changamoto za gharama na upatikanaji wa makazi.

Kupitia mpango huu, wateja wa Benki ya Exim watafaidika na mikopo ya hadi TZS 1 bilioni chini ya Personal na Preferred Banking, na hadi TZS 1.5 bilioni chini ya Elite Banking, ikiwa na makubaliano nafuu ya riba.

“Kumiliki nyumba ni moja ya mafanikio makubwa kwa Watanzania wengi,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim Tanzania Andrew Lymo.

 “Kupitia ushirikiano wetu na Simba Developers, tunarahisisha safari ya ununuzi wa nyumba kwa kutoa mkopo kwa kadri ya uwezo wako, na kufanya urahisi kwa Watanzania wengi zaidi kufanikisha ndoto zao za kumiliki nyumba.”

Mkurugenzi wa Simba Developers Yusuf Hatimali Ezzi, aliongeza, “Nyumba zetu zimejengwa ili kutoa makazi ya kisasa, salama na ya viwango bora.

Kwa kushirikiana na Benki ya Exim tunahakikisha wanunuzi wetu wanaweza kupata fedha kwa haraka na kwa urahisi, na kusaidia familia nyingi ziweze kuishi kwenye nyumba ya ndoto zao.”

Ushirikiano huu unaimarisha nafasi ya Benki katika soko la mikopo ya makazi wakati mahitaji ya huduma za kifedha za makazi kwa ajili ya  wateja yanaendelea kuongezeka.

Urahisishwaji wa mikopo ya nyumba Benki ya Exim Tanzania na Simba Developers wameongeza  viwango vya upatikanaji wa makazi bora na ya kisasa kwa Watanzania.

Aidha, hii inathibitisha dhamira ya Benki hiyo, katika maendeleo ya taifa kwa kupanua upatikanaji wa mikopo ya makazi na kusaidia ukuaji wa makazi bora.

Kwa wateja wa Benki hiyo, ushirikiano huu unarahisisha upatikanaji wa mikopo ya nyumba, chaguzi sahihi za fedha, na kurahisisha upatikanaji wa nyumba za kisasa kwa mtindo wowote wa maisha na gharama rafiki, Exim Bank na Simba Developers wanawawezesha Watanzania wengi kufanya maamuzi ya kumiliki nyumba kwa kujiamini, kuboresha usalama wao wa kifedha na ustawi wa familia zao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments