Wednesday, March 25, 2026
spot_img
HomeBiasharaCRDB yabainisha mkakati uwezeshaji wanawake katika biashara

CRDB yabainisha mkakati uwezeshaji wanawake katika biashara

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori, amehudhuria mjadala wa Wanawake katika Biashara na Mitandao ya Ugavi uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa Shirika la Fedha (IFC) wa Washirika wa Kimataifa wa Biashara uliendelea Lisbon, Ureno.

Akizungumza katika mjadala huo, Profesa Mori amesisitiza kwamba uwezeshaji wa wanawake ni sehemu muhimu ya mkakati wa muda wa kati wa Benki ya CRDB katika kuendeleza uchumi. Amebainisha kuwa Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 800 katika kufadhili biashara zinazoongozwa na wanawake, hatua inayogusa zaidi ya wanawake milioni 1 kote nchini.

Uwezeshaji huu unafanyika kupitia suluhisho bunifu kama CRDB Malkia na programu jumuishi zinazotekelezwa na CRDB Bank Foundation kupitia Programu ya IMBEJU, ikijumuisha elimu ya fedha, mafunzo ya ujasiriamali, na kuunganisha wanawake na fursa za kimasoko.

Aidha, Profesa Mori amesisitiza juhudi za Benki katika kufungua masoko mapya kwa wanawake, ikiwemo uwezeshaji wa kushiriki katika biashara za kikanda na Soko Huru la Afrika. Mkakati huu unahusisha pia uwekezaji katika sekta muhimu kama kilimo, biashara, miradi endelevu ya kijani, pamoja na miradi ya nishati safi ya kupikia, kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika uchumi unaojali mazingira na maendeleo endelevu.

Profesa Mori ameeleza kuwa CRDB kupitia ubunifu, ushirikiano, na uwekezaji wenye tija inaendelea kufungua milango ya mafanikio kwa wanawake Tanzania na barani Afrika kwa ujumla, ikithibitisha nafasi ya Benki kama kiongozi wa ajenda ya ujumuishi wa kiuchumi na kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa mitaji na maarifa ya biashara.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments