Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi, amesema Kanisa Katoliki halina ugomvi wowote na serikali na halina mpango wa kupigana nayo mieleka.
Askofu Ruwa’ichi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo kwenye Misa ya Jubilei ya Mapadri wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Msimbazi Centre.
Askofu huyo ameyasema hayo kufuatia kusambaa kwa kipeperushi kilichodaiwa kusambazwa na uongozi wa Jimbo kikidai kuwapo kwa misa katika siku ya Oktoba 29 ambayo ni ya kupiga kura.
“ Taarifa ile haikutoka ofisini kwangu na wala si ya jimbo. Kabisa halina ugomvi wowote na serikali. Tuwe makini na taarifa za upotoshaji”




