
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza muda wa siku tatu wa maombolezo ya kitaifa kufuatia mkasa wa moto uliowaka katika bweni la Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri na kusababisha vifo vya watoto 18.
Katika tangazo lililotolewa na ofisi ya Ijumaa jioni, rais huyo wa Kenya kuwa siku hizo tatu zitaanza alfajiri Jumatatu, Septemba 9, hadi machweo siku ya Jumatano, Septemba 11, 2024.
Bw Ruto ameagiza kuwa katika kipindi hiki, bendera za Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki zipeperushwe nusu mlingoti kote nchini.
“Kwa masikitiko makubwa na heshima ya kumbukumbu ya maisha ya watu wasio na hatia waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa katika mkasa huu, mimi, William Samoei Ruto, chini ya mamlaka niliyopewa kama Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amiri Jeshi Mkuu.




Vikosi vya Ulinzi vya Kenya, vinatoa agizo hili na kuelekeza kwamba, kama ushuhuda mzito wa alama isiyofutika iliyoachwa katika ufahamu wa taifa na roho za watoto kumi na saba walioaga, Kenya itaadhimisha muda wa siku tatu wa maombolezo ya kitaifa,†likasoma tangazo hilo.
“Katika kipindi hiki cha maombolezo ya kitaifa, Bendera ya Jamhuri ya Kenya na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) itapeperushwa nusu mlingoti Ikulu, Balozi zote za Kenya, Majengo ya Umma, Viwanja vya Umma , Vituo vyote vya Kijeshi, Vituo, Vituo, Meli zote za Wanamaji za Jamhuri ya Kenya, na katika eneo lote la Jamhuri ya Kenya, kuanzia alfajiri ya Jumatatu, tarehe 9 Septemba 2024 hadi machweo ya Jumatano, tarehe 11 Septemba 2024.â€

Rais alielezea huzuni ya pamoja ya taifa, akitoa salamu zake za rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto wao kwa moto.
“Tukio hili linatulazimisha kuhakikisha uwajibikaji katika shule zote nchini na kuchukua kila hatua tuwezayo kulinda maisha ya watoto wetu wanaokwenda shule. Hakuna mtoto anayepaswa kupoteza maisha katika sehemu ambayo imekusudiwa kuwa kimbilio salama kwa elimu, ukuaji na maendeleo ya kijamii,†alisema.
Chanzo: BBC Swahili