Sunday, November 2, 2025
spot_img
HomeAfyaMagonjwa ya moyo yatajwa kuongoza vifo Tanzania

Magonjwa ya moyo yatajwa kuongoza vifo Tanzania

Mratibu wa Huduma za Ukimwi Mkoa wa Dar es Salaam, Ayubu Kibao, amesema magonjwa ya moyo yamekuwa tatizo sugu linalosababisha vifo vya Watanzania wengi, hivyo jamii inapaswa kuyachukulia kwa uzito na umakini mkubwa.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 15 ya Hospitali ya Heameda jijini Dar es Salaam, Kibao alisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa (NCDs), ikiwemo moyo, saratani na figo, ambayo yanaongezeka kwa kasi nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda, ambaye pia ni Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Dkt. Hery Mwandolela, alisema magonjwa hayo husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo nchini na duniani.

“Kila mwaka, watu zaidi ya milioni 20 hufariki dunia kutokana na magonjwa ya moyo na saratani. Haya ni magonjwa yanayozuilika endapo jamii itachukua hatua mapema kwa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara,” alisema Dkt. Mwandolela.

Aliongeza kuwa ni muhimu Watanzania kubadili mitindo ya maisha, kuepuka ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kujenga tabia ya kupima afya mapema.

Hospitali ya Heameda imeendelea kutoa elimu na huduma za uchunguzi wa mapema, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza athari za magonjwa yasiyoambukizwa nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments