Klabu ya Mbeya City imekaribisha kwa furaha hatua ya Shirikisho la Soka (TFF) kufungua upya Uwanja wa Sokoine baada ya ukarabati wa sehemu ya kuchezea.
Ofisa Mtendaji Mkuu, Ally Nnunduma, amesema kurejea nyumbani kutawapa mashabiki burudani ambayo wameikosa kwa muda kwani timu imekuwa ikitumia KMC Complex jijini Dar.




