Mchengerwa: Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha vifo vya Wajawazito vinavyotokana na matatizo ya uzazi kutoka wastani wa Vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 (Mwaka 2015/2016) hadi kufikia wastani wa vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 (Mwaka 2022).

Amesema vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 (mwaka 2015/2016) hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 (Mwaka 2022).

“Tunamshkuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya uliopelekea kupungua kwa kiwango kikubwa vifo vya mama wajawazito vinavyotokana na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.”-Mchengerwa

Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa kukabidhi vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Watoto Njiti) na watoto wachanga wagonjwa na wenye uzito pungufu.

Vifaa na vifaa tiba hivyo vimetolewa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation kwenye hospitali ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *