Mgunda aondoka Klabu ya Simba

Klabu ya Simba Sc imethibitisha kuwa Kocha Juma Ramadhani Mgunda hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya Wanawake wa Simba Queens baada ya mkataba wake kutamatika na kubainisha kuwa kikosi hicho kwa sasa kitakuwa chini ya Kocha msaidizi, Mussa Hassan Mgosi ambae tayari ameshaanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ambayo itaanza hivi karibuni

Katika kipindi chake klabuni hapo Kocha Mgunda ameiwezesha Simba Queens kurejesha taji lake la ligi kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).

“Uongozi wa Simba unapenda kumshukuru Kocha Mgunda kwa utumishi wake ndani ya klabu yetu akianza kukitumikia kikosi cha Simba cha Wanaume (Simba Senior Team) kisha kuham- ishiwa timu ya Wanawake (Simba Queens) na kote akitimiza vema majukumu yake.” imesema taarifa ya Simba SC

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *