Sunday, November 2, 2025
spot_img
HomeHabariMkuu wa usalama CHADEMA ahamia CCM, afichua njama hatari za upinzani

Mkuu wa usalama CHADEMA ahamia CCM, afichua njama hatari za upinzani

Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Nyamatari Tengecha amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema hataki kuendelea kuwa sehemu ya wanaharakati wanaopelekwa nje ya nchi kupewa mafunzo ya kijeshi ili kuiharibu amani ya Tanzania.

Sambamba na hilo, amesema katika maisha yake ndani ya CHADEMA, amezifahamu asasi kutoka nje ya nchi, zinazokifadhili chama hicho na wanaharakati ili kuiharibu amani na usalama wa nchi.

Dk Tengecha ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Oktoba 28, 2025 alipozungumza baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Mgombea urais wa chama hicho, Dk Samia Suluhu Hassan, jijini Mwanza.

“Kuna watu hawataki mazuri ya nchi yetu najua wanapata wapi fedha, kila kitu ninakifahamu, ninajua asasi za nje zilizokuwa zinatupatia fedha mpaka saa hizi kuharibu usalama wa nchi yetu,” amesema.

Amesema ameondoka Chadema ili kujitenga na wanaharakati waliokuwa wanawachukua na kuwapeleka nje ya nchi kuwapa mafunzo ya kijeshi ili waharibu amani ya nchi.

“Sitaki kuendelea kuwa sehemu ya wanaharakati wanaotuchukua na kutupeleka Nairobi na kwingine kote kupata mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kuharibu amani ya nchi yetu,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments