Wednesday, March 25, 2026
spot_img
HomeHabariMUWSA yatangaza dau la milioni mbili atayetoa taarifa wizi mita za maji

MUWSA yatangaza dau la milioni mbili atayetoa taarifa wizi mita za maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi imetangaza zawadi ya Sh. milioni mbili kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini watu wanaohujumu miundombinu ya maji katika maeneo yake ya huduma.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya wizi wa mita za maji, viungio vyake, mifuniko ya chemba za maji pamoja na gate valve, hali inayosababisha hasara kubwa kwa mamlaka hiyo na serikali kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, takribani mita 266 zimeibwa kuanzia Januari hadi Machi 2026 katika kata za Makuyuni, Njiapanda, Majengo, Mwika Kaskazini na maeneo ya jirani. Matukio hayo yameisababishia serikali hasara inayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 37.2.

Mamlaka imewahakikishia wananchi kuwa taarifa zote zitakazotolewa zitahifadhiwa kwa siri kubwa ili kulinda usalama wa watoa taarifa na kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.

Sambamba na hilo, wananchi wametakiwa kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0791 992 525, ambayo imewekwa maalum kwa ajili ya kuripoti vitendo hivyo vya hujuma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments