Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariNiffer, Mika Chavala wafikishwa tena Kisutu kuendelea na kesi ya Uhaini

Niffer, Mika Chavala wafikishwa tena Kisutu kuendelea na kesi ya Uhaini

Jenifer Jovin maarufu kama Niffer, Mika Chavala na wenzao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Desemba 3, 2025 kwa ajili ya kuendelea na shauri la Uhaini linalowakabili.

Washtakiwa hao wamekuwa wakikabiliwa na kesi hiyo kwa muda sasa, ikiwa ni mfululizo wa hatua za kisheria zilizoanza baada ya kukamatwa kwao wakidaiwa kujihusisha na vitendo vinavyodaiwa kuhatarisha usalama wa taifa. Kesi yao imekuwa ikivuta hisia za umma kutokana na uzito wa mashitaka na umaarufu wa baadhi ya washtakiwa katika mitandao ya kijamii na shughuli za kijamii.

Katika muendelezo wa shauri hilo leo, washtakiwa waliwasilishwa mahakamani kwa utaratibu wa kawaida huku upande wa mashtaka na ule wa utetezi ukiendelea na hatua za awali za usikilizwaji wa mashahidi na vielelezo. Hata hivyo, upande wa mahakama bado unaendelea kupitia nyaraka mbalimbali na kupanga tarehe za hatua zinazofuata katika mwenendo wa kesi.

Mashabiki, ndugu na wafuasi wa washtakiwa hao waliendelea kufuatilia mwenendo huo kwa karibu, wakisubiri kwa hamu maendeleo ya kesi ambayo bado ipo katika hatua za awali za usikilizwaji.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments