
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kuwashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mama na bintiye wakazi wa mkoani humo
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Alchelaus Mutalemwa amewataja watu hao ambao ni Daudi Elias Nyakongo (45), Rajabu Rashidi (45) na Fikiri Steven (45) wote ni wakazi wa Kata ya Mkonze.
Kamanda Mutalemwa amesema kuwa watuhumiwa wanahojiwa na uchunguzi ukikamilika, watafikishwa mahakamani.
