Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeBiasharaPPP yatajwa kuongeza uwekezaji na kuchochea ukuaji wa viwanda

PPP yatajwa kuongeza uwekezaji na kuchochea ukuaji wa viwanda

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa PPP Centre, Flora Tenga, amesema kuimarisha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) ni msingi muhimu wa kuvutia uwekezaji na kukuza viwanda vinavyochangia pato la Taifa.

Akizungumza katika Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPD) yaliyofanyika Novemba 27, 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Tenga alisema sekta ya viwanda ni nguzo kuu ya uchumi na mafanikio yake yanategemea mifumo madhubuti ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.

Tenga alisema PPP inaharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa inayohitaji rasilimali na utaalamu wa pande zote, hivyo kupanua fursa za ajira na kuongeza tija kwenye sekta ya viwanda.

“Ubia huu unawawezesha wawekezaji kushirikiana na serikali katika miradi yenye changamoto za miundombinu, na ni njia bora ya kuongeza ukuaji wa viwanda na mchango wake kwenye uchumi,” alisema Tenga.

Aidha, alihimiza wadau waongeze ushirikiano katika miradi mikubwa ya Express Way za Kibaha–Chalinze na Chalinze–Morogoro, akibainisha kuwa utekelezaji wake utachochea maendeleo na kuvutia uwekezaji katika Mkoa wa Pwani.

Mdahalo huo ulihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Pili Mnyema (aliyemwakilisha RC Abubakar Kunenge), Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri, uongozi wa CTI, pamoja na wadau kutoka taasisi za serikali ikiwa ni pamoja na TISEZA na STAMICO, pamoja na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments