Thursday, February 12, 2026
spot_img
HomeHabariRais Dk.Mwinyi awasili Maputo kushiriki miaka 50 ya Siku ya Ushindi nchini...

Rais Dk.Mwinyi awasili Maputo kushiriki miaka 50 ya Siku ya Ushindi nchini Msumbiji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Maputo, Msumbiji akitokea nchini Indonesia kwa gwaride maalum na ujumbe wake akiwemo Mkewe Mama Mariam Mwinyi.

Katika uwanja wa ndege wa Maputo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji akiwemo Waziri wa Afya wa nchi hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi atashiriki Sherehe za Miaka 50 ya Siku ya Ushindi nchini Msumbiji.

Kuhudhuria kwake katika sherehe hizo kunatokana na mualiko Maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments