Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika matukio tofautitofauti alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa Nchini Ethiopia leo February 14, 2025 kwaajili ya kushiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Rais Dkt. Samia pia atashiriki mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.







