Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariSeth Msangwa Mwenyekiti Mpya Halmashauri ya Shinyanga

Seth Msangwa Mwenyekiti Mpya Halmashauri ya Shinyanga

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamemchagua Diwani wa Kata ya Imesela Seth Anthony Msangwa, kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo, akichukua nafasi ya aliyemaliza muda wake Ngassa Mboje.

Uchaguzi huo umefanyika leo Desemba 2, 2025, mara baada ya madiwani kupishwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Nido, Olivia Bisaga.

Akitangaza matokeo, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga, amesema jumla ya wapiga kura walioandikishwa ni 38, lakini waliopiga kura ni madiwani 36, na wote wamemchagua Seth Msangwa kwa kura za ndiyo.

Kitinga ameongeza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti pia imekwenda kwa kura zote 36 kwa Joseph John Buyugu.

“Kwa mamlaka niliyopewa, namtangaza Seth Anthony Msangwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na Joseph John Buyugu kuwa Makamu Mwenyekiti,” amesema Kitinga.

Baada ya uchaguzi huo, Halmashauri iliunda kamati mbalimbali za kudumu zitakazohusika na usimamizi wa majukumu ya kisheria na kiutendaji ya Halmashauri.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments