Friday, December 5, 2025
spot_img
HomeHabariRais Samia: Vurugu zimeratibiwa, walitaka kupindua nchi

Rais Samia: Vurugu zimeratibiwa, walitaka kupindua nchi

Rais Samia Suluhu Hassan amesema vurugu za Oktoba 29, zilipangwa, kugharimiwa na kuratibiwa na watu kutoka nje, huku dhamira yao ikiwa ni kiupindua nchi.

“Lile lilikuwa ni jambo la kupangwa na vurugu zile zilidhamiria makubwa. Vurugu zile ni mradi wenye nia ovu wenye wafadhili, washitiri na watekelezaji.

“Wapo walioingia kwa kufuata mkumbo tu pengine kwa ahadi ya maisha mazuri baadaye,” amesema.

Sambamba na hilo, amesema vurugu hizo ziliratibiwa na watu wanaoishi nje ya nchi, wapo wanaojulikana na wengine hawajulikani, hivyo Serikali inawatafuta ili kuwajua.

“Hili ambo lina waratibu kutoka nje, lakini kwanini waratibu kutoka nje. Wale waratibu kutoka Tanzania tunawajua, ni shida za maisha, akisukuma maandamano umbea watanzania wale wale vijana wanatumia fedha zao kununua bando kuwasoma yeye ukisoma wanapata fedha,” amesema.

Amesema wapo ambao hawana shida ya maisha wako pazuri wanalipwa kwa sababu wamekosa uzalendo na ukiwatazama vizuri sio Watanzania kamili.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Desemba 2, 2025 katika hotuba yake kwa Taifa, wakati wa kikao chake na wazee wa Jiji la Dar es Salaam.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments