Burudani ya muziki wa Hiphop, iliyoimbwa na Mgombea ubunge wa Nachingwea, Fadhili Liwaka katika jukwaa la kampeni, zimemuibua Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, aliyeshindwa kujizuia na kuanza kucheza.
Hilo limeshuhudiwa leo, Jumatano Septemba 24, 2025 katika mkutano wa kampeni za urais Ruangwa mkoani Lindi.
Liwaka alianza kuimba muziki huo, alipokuwa jukwaani kuomba kura, huku Dk. Samia akicheza katika jukwaa kuu.




