Timu ya Taifa ya tenisi kwa watu wenye ulemavu inaendelea na mazoezi kujiandaa na mashindano ya wazi yatakayoanza Septemba 8, Nairobi, Kenya.

Kocha Mkuu, Riziki Salum, alisema kila mchezaji anajituma kuhakikisha bendera ya taifa inapepea vema. Timu itaondoka Septemba 6, huku akieleza kuridhishwa na viwango vya wachezaji na kuishukuru serikali kwa sapoti.




