Sunday, January 25, 2026
spot_img
HomeMichezoSimba Queens yaifuata Yanga Princess Nigeria

Simba Queens yaifuata Yanga Princess Nigeria

Baada ya Yanga Princess kumsajili beki wa kati raia wa Nigeria, Ogbona Akudo, wapinzani wao wa jadi Simba Queens nao wameelekea nchini humo kusaka saini ya Odoma Amarachi, kiraka wa Edo Queens.

Amarachi, aliyecheza timu ya taifa ya Nigeria na kushiriki ubingwa wa WAFCON nchini Morocco, amekubali kujiunga na Simba Queens na kinachosubiriwa ni taratibu za mwisho kabla ya kutua nchini.

Mchezaji huyo ni kiraka mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi—kiungo mkabaji, mshambuliaji na beki zote mbili, huku akitumia miguu yote miwili.

Simba Queens, ambayo imewaacha zaidi ya wachezaji 11, ipo kwenye mchakato wa kujenga kikosi kipya chenye wachezaji wa timu za taifa. Tayari imemalizana na winga wa Kampala Queens ya Uganda, Zainah Nandede, mastraika Cynthia Musungu Shilwatso (Kenya) na Zawadi Usanase (AS Kigali, Rwanda), pamoja na beki wa kushoto wa Yanga Princess, Asha Omary.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments