Thursday, December 11, 2025
spot_img
HomeMichezoTFF yamteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu

TFF yamteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemteua Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo, Oscar Mirambo, kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Kidao Wilfred ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika Septemba 30, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, uteuzi wa Mirambo utaanza rasmi Oktoba 1, 2025, huku akihesabika rasmi kuwa mtendaji mkuu wa shirikisho hilo kwa muda wa mpito hadi mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya utakapokamilika.

Mirambo ni miongoni mwa wataalamu wa soka wenye uzoefu mkubwa nchini, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya TFF ikiwemo kocha wa timu za vijana na baadaye kuongoza Idara ya Ufundi.

Uongozi wa TFF umeeleza kuwa unampongeza Kidao Wilfred kwa mchango wake mkubwa katika kipindi chote cha utumishi wake, hususan katika masuala ya kiutawala na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

Kwa uteuzi huu, Mirambo atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli zote za kiofisi na kiutendaji ndani ya TFF sambamba na kuhakikisha shirikisho linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa mujibu wa katiba.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments