TRA United imerejea kwa nguvu kwenye Ligi Kuu baada ya kupata ushindi wake wa kwanza wa msimu kwa mabao 1–0 dhidi ya Prisons katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Kocha Kassim Otieno alisema timu imefanya marekebisho muhimu kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA na sasa iko tayari kuendelea na ushindi.
“Tumerudisha ari na naamini huu ni mwanzo mzuri. Tutapambana kuhakikisha tunadumisha ushindi,” alisema Otieno.
Awali, TRA United ilikuwa haijapata ushindi katika mechi tatu, ikitoka sare dhidi ya Dodoma Jiji, Pamba Jiji na Mashujaa FC. Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 55 na Ramadhani Salum ‘Chobwedo’, likiifanya timu kupanda hadi nafasi ya 10 ikiwa na pointi sita.
Kwa upande wa Prisons, kichapo hicho ni cha tatu msimu huu na kinawaacha nafasi ya 11 baada ya mechi tano.




