Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeBiasharaWakulima wa ufuta wafurahia mbegu bora za bure

Wakulima wa ufuta wafurahia mbegu bora za bure

Wakulima wa ufuta mkoani Lindi wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kwa kuwapatia tani saba za mbegu bora za ufuta, zilizokabidhiwa kwa uongozi wa mkoa kwa ajili ya kugawiwa bure kwa wakulima.

Wamesema hatua hiyo itawapa hamasa ya kuendeleza kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji katika msimu huu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amesema mbegu hizo zitasambazwa katika halmashauri zote sita za mkoa huo ikiwa ni jitihada za serikali kuimarisha uzalishaji wa ufuta. Amewataka maafisa ugani kusimamia kwa karibu shughuli za kilimo ili kuongeza tija na ubora wa mazao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Irene Mlola, amesema mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia nafaka na mazao mchanganyiko kama ufuta, mbaazi na choroko, na kwamba hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wakulima kuongeza uzalishaji.

Makabidhiano ya mbegu hizo, zinazofikia kilo 7,000, yalifanyika Novemba 18 katika viwanja vya maonesho ya Nane Nane, Ngongo, mjini Lindi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments