Sunday, November 2, 2025
spot_img
HomeHabariWamachinga, maofisa usafirishaji Dar wahamasisha ushiriki upigaji kura

Wamachinga, maofisa usafirishaji Dar wahamasisha ushiriki upigaji kura

Umoja wa Wamachinga pamoja na Maafisa Usafirishaji wa Pikipiki na Bajaji wa Mkoa wa Dar es Salaam wameahidi kushiriki kwa wingi kupigakura, wakisisitiza kuwa ni haki ya kikatiba na njia sahihi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo Tanzania (Wamachinga) Mkoa wa Dar es Salaam, Steven Lusinde, amesema hayo leo mjini Ilala wakati akizungumza na waandishi wa habari. Lusinde pia amewatahadharisha wananchi kutojihusisha na watu wachache wenye nia mbaya ya kuvuruga amani wakati wa uchaguzi.

“Ni muhimu kila Mtanzania kutumia haki yake ya kikatiba kwa amani. Tusikubali kushawishiwa na wale wanaotaka kuleta vurugu au kuchochea migogoro bila sababu za msingi,” amesema Lusinde.

Aidha, Lusinde amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi ni hatua muhimu ya kuimarisha demokrasia na kuleta maendeleo ya kweli kwa taifa. Amesisitiza, “Tushiriki kikamilifu katika zoezi la kuchagua viongozi tunaowataka, ili tuwe sehemu ya maamuzi ya kuijenga nchi yetu.”

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments