Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariWaziri Aweso aikazia DAWASA kuharakisha huduma ya maji Msakuzi, atoa siku 30

Waziri Aweso aikazia DAWASA kuharakisha huduma ya maji Msakuzi, atoa siku 30

 Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ametoa maagizo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mkama Bwire, kuhakikisha huduma ya maji inapelekwa kwa wakazi wa Msakuzi, katika shina namba tano na saba, ndani ya siku 30. 

Maagizo hayo yalitolewa Novemba 27,2025 baada ya Waziri Aweso kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, waliodai kuwa licha ya kuwepo kwa miundombinu ya maji, bado hawapati huduma hiyo kwa uhakika. 

Waziri Aweso amewataka viongozi wa DAWASA kuchukua hatua za haraka ili kutatua tatizo hilo na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama. 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments