Tuesday, March 24, 2026
spot_img
HomeMichezoYanga SC: Bado tuko vitani kurejesha dozi

Yanga SC: Bado tuko vitani kurejesha dozi

Licha ya kusuasua katika michezo mitatu mfululizo, Yanga imesema inajivunia rekodi ya kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa haijapoteza mechi hata moja, huku pia ikiwa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 38 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 31, lakini Mnyama amecheza mechi mbili pungufu.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema msimu huu wamefanya vizuri zaidi tofauti na ilivyokuwa katika msimu uliopita.

Kamwe amesema wanawapongeza wachezaji wao kwa juhudi wanazozionesha katika kusaka matokeo mazuri licha ya ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo pamoja na ‘lundo’ la majeruhi.

Amesema kwa kuangalia hayo, wanawaomba wanachama na mashabiki kutulia kwa sababu  bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu kama nyota wao ambao ni majeruhu watarejea dimbani.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments