Zinedine Zidane atamrithi, Didier Deschamps, kama Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ufaransa wakati wa majira ya joto, huku makubaliano ya ‘mdomo’ tayari yamefikiwa kati ya nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), vyanzo vimeiambia ESPN.
Kuondoka kwa Deschamps katika kikosi cha Ufaransa baada ya miaka 14 ya mafanikio kumekuwa na siri iliyofichwa zaidi katika soka la nchi hiyo na Zidane, ambaye alimaliza muda wake wa pili kama Kocha wa Los Blancos mwaka 2021.
Akiwa na umri wa miaka 53, Zidane alikuwa akimsubiri mshindi mwenzake wa Kombe la Dunia mwaka 1998 aondoke ili achukue nafasi hiyo.
Amelazimika kusubiri kwa muda mrefu kuliko alivyofikiria mwanzoni, lakini atateuliwa rasmi mara tu Fainali za Kombe la Dunia la mwaka huu litakapokamilika.
Maelezo ya mwisho ya kufafanua kabla hajasaini mkataba wake ni kuhusu wafanyakazi wake na jinsi timu yake inaweza kuwa kubwa.




