
Mwanasiasa mashuhuri Nchini Uganda ambaye pia ni Rais wa NUP, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na Polisi wakati Polisi wakiwatawanya Wafuasi wake katika eneo la Bulindo Manispaa ya Kira.
Vyombo vya Habari Nchini Uganda vimeripoti kuwa Bobi amepigwa risasi mguuni kauli ambayo imethibitishwa na Admin wa ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Bobi Wine ambaye amekiri Bobi amepigwa risasi na amefikishwa Hospitali kupata matibabu.
