Wednesday, February 4, 2026
spot_img
HomeHabariCoca-Cola yazindua kampeni ya 'Food Pass' yenye zawadi kemkem kwa wateja wa...

Coca-Cola yazindua kampeni ya ‘Food Pass’ yenye zawadi kemkem kwa wateja wa KFC Dar es Salaam 

Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imezindua kampeni maalum inayowalenga wateja wa migahawa ya KFC jijini Dar es Salaam, ambapo wanapata fursa ya kushiriki Tamasha la Chakula la Coca-Cola linalotarajiwa kufanyika Novemba sambamba na zawadi kemkem kutoka Coca-Cola.

Kampeni hiyo, iitwayo ‘Food Pass’, inatoa zawadi mablimbali kwa wateja watakaonunua chakula maalum cha “Pamoja-Coke Fest Meal”, ambacho kinajumuisha vipande vinne vya kuku, chipsi, na Coca-Cola.

Wateja watakaonunua chakula hicho katika vituo vya KFC  ikiwemo Mlimani City, Mikocheni Plaza, Mbezi Beach, Magomeni, Diamond Plaza, na Kariakoo wataweza kujisajili kwa ajili ya kupata kijitabu cha ‘Food Pass’. Kijitabu hiki kitawapa fursa ya kuingia bure kwenye tamasha la kufunga Coca-Cola Food Fest litakalofanyika mwezi Novemba.

Kila mteja anapopata chakula hiki, kijitabu chake cha ‘Food Pass’ kitapigwa muhuri, na mihuri hiyo itafungua zawadi mbalimbali, huku wateja 1,000 wa kwanza wakipata tiketi za bure za kuingia kwenye tamasha. Kampeni hii itafanyika kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 22.

Kabula Nshimo, Meneja wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania, alisema kuwa kampeni hii ni sehemu ya muendelezo wa Coca-Cola Food Fest inayoadhimisha vyakula mbalimbali na bidhaa za Coca-Cola kote nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments