Wednesday, February 18, 2026
spot_img
HomeBiasharaCRDB Bank Foundation yakabidhi Sh. bilioni 2, pikipiki 20 Mtumba

CRDB Bank Foundation yakabidhi Sh. bilioni 2, pikipiki 20 Mtumba

Taasisi  ya CRDB Bank Foundation imetenga Sh. bilioni 2 kufanikisha miradi na biashara za wanachama wa Umoja wa Wanawake na Samia, vijana na wajasiriamali katika Jimbo la Mtumba mkoani Dodoma.

Akikabidhi mfano wa hundi wa shilingi bilioni 2 pamoja na pikipiki 20 kwa wanawake na vijana, Waziri wa Madini ambaye ni Mbunge wa Mtumba, Mheshimiwa Anthony Mavunde, ameipongeza CRDB Bank Foundation kwa dhamira yake ya dhati ya kuwainua wanawake na vijana ambao ni kundi kubwa la nguvukazi nchini akisema inaunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.

“Uwezeshaji huu utaongeza kasi ya uanzishaji na ukuzaji biashara changa na ndogo hali itakayochochea ajira na kuongeza kipato binafsi, kuimarisha uchumi wa kaya na kuchangi amapato ya serikali hasa kwa wanawake na vijana ambao ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa,” amesema Waziri Mavunde.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema uwezeshaji wa wanawake na vijana ni sehemu ya mkakati wanaoutekeleza kwa kuwapa wahusika mitaji wezeshi, mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha kupitia Programu ya iMbeju.

“Lengo la kuanzishwa kwa Taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation ni kufungua fursa kwa wanawake na vijana wajasiriamali. Wakati wote sisi tunawaza kuhusu namna ya kufanikisha hilo. Leo ni zamu ya Wanawake na Samia pamoja na vijana wa Jimbo la Mtumba. Mipango na mikakati yetu ni kuwafikia wajasiriamali kote nchini,” amesema Tully.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments