
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza maboresho ya ratiba ya Ligi kuu ya NBC, ikiwemo kupanga tarehe kwa michezo 14 ambayo haikuwa na tarehe hapo awali.
Miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na mechi ya Simba SC dhidi ya Yanga SC ambayo itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya KMC, huku tarehe ikibaki Oktoba 19, 2024.