
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Maji Ibihwa, Wilayani Bahi, Jijini Dodoma.
Mpango ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri na utejelezaji wa miradi ya maji nchini.
Pamoja na hilo pongezi hizi zimejukisha mradi wa maji Ibihwa na kusisitiza kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima ili Wananchi wapatie huduma ya Majisafi na kwamba ahadi ya kukamilisha mradi wa Ibihwa ifikapo tarehe 30.09.2024 itekelezwe kwa wakati.
Aidha akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa Maji (Mb.), Jumaa Hamidu Aweso amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Ibihwa kuwa, Wizara itakamilisha mradi huo kabla ya tarehe 30/09/2024 na kwamba Maji yatafika pia katika Mji wa Bahi.
Mradi wa Maji Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ukiwa umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na umeanza kutoa huduma kwa Wananchi, ambapo mradi huu utawanufaisha wananchi wapatao 8,932 wa Kijiji cha Ibihwa.