Fadlu, Ahoua bora Agosti

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amechaguliwa kuwa kocha bora wa Ligi Kuu Bara wa mwezi Agosti huku nyota wa timu hiyo, Jean Charles Ahoua akichaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya mwezi huo.

Fadlu amewapiga chini Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdalah Mohamed wa Mashujaa alioingia nao fainali baada ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini kuiongoza Simba kuvuna pointi sita katika mechi mbili ilizocheza ikifunga mabao saba bila ya wavu wao kuguswa.

Kiungo wa boli,Ahoua aliiwezesha timu yake kupata ushindi katika mechi mbili ilizocheza, akifunga bao moja na kuhusika kupika mabao mengine (asisti) tatu.

Aidha, kamati ya tuzo imemtangaza meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Ashraf Omary kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Agosti.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *