Wednesday, March 25, 2026
spot_img
HomeGeneral NewsHomera apongeza mifumo ya kidigitali Chuo cha Uongozi wa Mahakama

Homera apongeza mifumo ya kidigitali Chuo cha Uongozi wa Mahakama

Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera, amepongeza maendeleo ya mifumo ya kidigitali ya ufundishaji katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kilichopo Lushoto.

Akizungumza wakati wa ziara yake chuoni hapo Machi 24, 2026, Dk. Homera alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika matumizi ya teknolojia ya kisasa kufundishia majaji, mahakimu na watumishi wengine wa mhimili wa mahakama.

Alieleza kuwa mifumo hiyo imeongeza ufanisi, uwazi na ubora wa mafunzo, hali inayochangia kuimarika kwa utoaji wa haki nchini.

“Kwa kweli nimefurahishwa sana na kiwango cha matumizi ya teknolojia hapa chuoni. Mifumo ya kidigitali imeboresha kwa kiasi kikubwa mbinu za ufundishaji na ujifunzaji. Hii ni hatua muhimu katika kujenga mahakama yenye weledi na ufanisi wa hali ya juu,” alisema Dk. Homera.

Aidha, alisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kituo bora cha umahiri si tu nchini bali pia barani Afrika, kwa kuzalisha wataalamu mahiri watakaohudumia sekta ya sheria kwa ufanisi.

Awali, akiwasilisha taarifa ya chuo, Mkuu wa chuo hicho, Paul Kihwelo, alisema taasisi hiyo imeendelea kuzalisha wataalamu wenye weledi kwa kuwapatia nyenzo muhimu za uendeshaji wa mashauri mahakamani.

Aliongeza kuwa kupitia mfumo wa kidigitali wa mafunzo kwa njia ya mtandao unaojulikana kama IJA e-LMS, chuo hicho kimefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi na kupanua wigo wa upatikanaji wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya sheria.

Mafanikio hayo, kwa mujibu wa Dk. Kihwelo, yanaakisi juhudi za Serikali katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika sekta ya sheria nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments