“Jasusi wa Urusi” akutwa amekufa Norway

Nyangumi aina ya ‘beluga’ anayeshukiwa kupewa mafunzo ya kijasusi na Urusi amekutwa amekufa pwani ya Norway.

Mwili wa nyangumi huyo -aliyepewa jina la utani kama Hvaldimir – ulikutwa ukielea na umepelekwa kwenye bandari ya karibu kwa uchunguzi.

Nyangumi huyo alionekana kwa mara ya kwanza katika maji ya Norway miaka mitano iliyopita, akiwa na kamera ya GoPro iliyofungwa kukiwa na picha zenye maandishi “Vifaa vya St Petersburg.”

Kufahamu zaidi kuhusu nyangumi Hvaldimir tembelea tovuti ya BBCSwahili.

Chanzo: BBCSwahili

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *