Mingange kuinoa Stand United FC

Mingange apewa mikoba ya Pluijm Azam | Mwanaspoti

ALIYEKUWA kocha wa Ndanda FC na Mashujaa, Meja Mstaafu Abdul Mingange, ametua katika timu ya Stand United ya Shinyanga ambayo itashiriki Ligi ya Championship msimu mpya.

Taarifa iliyotolewa na Stand United, inasema wamempa Mingange mkataba wa mwaka mmoja na wanaamini anauwezo wa kusaidia kuipandisha daraja timu hiyo iliyoteremka msimu wa 2018/19.

“Mingange ndiyo kocha wetu mpya, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu yetu,” ilisema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Mbali na kocha huyo, Stand United imemtangaza Daudi Macha kuwa kocha msaidizi, Ally Shomari (kocha wa makipa), na kipa wa zamani wa Moro United, JKT Ruvu, Ndanda, Coastal Union, Azam na Yanga, Jackson Chove, kuwa meneja wa timu.

Tayari Stand United imewasajili wachezaji kwa wapya kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi ambao ni pamoja na John Mwanda, Ally Hamisi, Mudrick Salim na Frank Sekule.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *