NeST yawezesha sekta ya manunuzi kuimarika-Simba

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) imewezesha kusomana kwa mifumo zaidi ya 17 iliyopo nchini kupitia mfumo mpya wa kieletroniki wa NeST kwenye sekta ya ununuzi wa umma.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA ,Denis Simba wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu Kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki linaloanza leo Septemba 9-12 Jijini Arusha na kushirikisha washiriki zaidi ya 500.

Amesema kupitia mfumo wa NeST umewezesha sekta ya manunuzi kuimarika zaidi katika usawa uwazi na ushindani katika sekta ya manunuzi.

“PPRA ni kinara wa mfumo wa NeST unaosimamia manunuzi na imefanikiwa kunganisha  mifumo zaidi ya 17 kupitia mfumo wa kieletroniki na Tanzania ni kinara katika kutekeleza  na kusimamia  ununuzi wa kidigitali “.amesema

Amesema NeST inarahisisha ununuzi wa umma,alisema kupitia kongamano hilo watabadilishana ujuzi na kupata uzoefu katika sekta ya manunuzi kwani Tanzania ni kinara katika kusimamia sekta ya manunuzi kupitia mifumo ya kieletroniki .

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *