Monday, February 16, 2026
spot_img
HomeBiasharaNMB yaitangaza Sekta ya Madini ya Tanzania Afrika Kusini

NMB yaitangaza Sekta ya Madini ya Tanzania Afrika Kusini

Benki ya NMB imewakilisha kikamilifu Tanzania katika maonesho ya uwekezaji ya Mining Indaba 2026, yaliyofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini, kuanzia Februari 8 hadi 11.

Kupitia maafisa wake waandamizi, waliongozwa na Nelson Karawa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa makampuni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Idara ya Hazina, Jeremiah Lyimo, NMB ilitumia jukwaa hilo kuitangaza Tanzania na sekta yake ya madini miongoni mwa wawekezaji wa kimataifa, ikisisitiza nafasi ya nchi yetu kama mojawapo ya maeneo yenye fursa lukuki za uwekezaji na rasilimali nyingi za madini duniani

Aidha, kama washiriki wengine kutoka Tanzania, NMB ilitumia fursa za mikutano na makongamano katika maonesho hayo kuonyesha ushiriki wake na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya madini nchini, pamoja na utayari wake wa kushiriki katika kufadhili miradi ya kimkakati ya madini.

Kwa kushirikiana na kampuni za Breakthrough Attorneys na Invest Africa, NMB iliandaa Mkutano wa Waevekezaji wa ‘Investing in Tanzania Mineral Value Chain Conference’. Mkutano huo ulilenga kuwatambulisha wawekezaji wa kimataifa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya madini hapa Tanzania na kuonesha kwamba mazingira ya biashara nchini tayari yameandaliwa kwa wawekezaji wa kimataifa.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini,James Bwana, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Madini, TISEZA, na Tume ya Madini.

Katika kongamano hilo, Lyimo alitumia fursa hiyo kuonesha na kueleza kuwa Benki ya NMB ina uwezo mkubwa wa kifedha pamoja na uzoefu wa kusimamia mikataba mikubwa. Pia, alisisitiza nafasi muhimu ya benki katika kuwezesha upatikanaji wa fedha kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya miradi mikubwa katika sekta ya madini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments